Native Bible

Mark 8:32 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Aliyasema haya waziwazi, ndipo Petro akamchukua kando na akaanza kumkemea.

Mark 8:32 in English

Mark 8:32 · Berean Standard Bible

He spoke this message quite frankly, and Peter took Him aside and began to rebuke Him.

Context

30Yesu akawaonya wasimwambie mtu yeyote habari zake. 31Ndipo akaanza kuwafundisha wanafunzi wake kuwa Mwana wa Adamu lazima atapata mateso mengi na kukataliwa na wazee, viongozi wa makuhani, na walimu wa sheria, na kwamba itampasa auawe lakini baada ya siku tatu afufuke. 32Aliyasema haya waziwazi, ndipo Petro akamchukua kando na akaanza kumkemea. 33Lakini Yesu alipogeuka na kuwaangalia wanafunzi wake, akamkemea Petro. Akasema, “Rudi nyuma yangu, Shetani! Moyo wako hauwazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.” 34Ndipo akauita ule umati wa watu pamoja na wanafunzi wake, akasema, “Mtu yeyote akitaka kunifuata, ni lazima ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake, anifuate.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.