Marko 8:14
Mark 8:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wanafunzi walikuwa wamesahau kuchukua mikate ya kutosha. Walikuwa na mkate mmoja tu kwenye mashua.
Mark 8:14 in English
Mark 8:14 · Berean Standard Bible
Now the disciples had forgotten to take bread, except for one loaf they had with them in the boat.
Context
12Akahuzunika moyoni, akawaambia, “Kwa nini kizazi hiki kinataka ishara? Amin nawaambieni, hakitapewa ishara yoyote.” 13Kisha akawaacha, akarudi kwenye mashua, akavuka hadi ngʼambo. 14Wanafunzi walikuwa wamesahau kuchukua mikate ya kutosha. Walikuwa na mkate mmoja tu kwenye mashua. 15Yesu akawaonya: “Jihadharini na chachu ya Mafarisayo na ya Herode.” 16Wakajadiliana wao kwa wao, na kusema, “Anasema hivi kwa sababu hatukuleta mikate.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.