Native Bible

Mark 6:50 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

kwa sababu wote walipomwona waliogopa. Mara Yesu akasema nao, akawaambia, “Jipeni moyo! Ni mimi. Msiogope!”

Mark 6:50 in English

Mark 6:50 · Berean Standard Bible

for they all saw Him and were terrified. But Jesus spoke up at once: “Take courage! It is I. Do not be afraid.”

Context

48Akawaona wanafunzi wake wanahangaika na kupiga makasia kwa nguvu, kwa sababu upepo ulikuwa wa mbisho. Wakati wa zamu ya nne ya usiku, Yesu akawaendea wanafunzi wake, akiwa anatembea juu ya maji. Alikuwa karibu kuwapita, 49lakini walipomwona akitembea juu ya maji, wakadhani ni mzimu. Wakapiga yowe, 50kwa sababu wote walipomwona waliogopa. Mara Yesu akasema nao, akawaambia, “Jipeni moyo! Ni mimi. Msiogope!” 51Akapanda ndani ya mashua nao, na ule upepo ukakoma! Wakashangaa kabisa, 52kwa kuwa walikuwa hawajaelewa kuhusu ile mikate. Mioyo yao ilikuwa migumu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.