Marko 6:49
Mark 6:49 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
lakini walipomwona akitembea juu ya maji, wakadhani ni mzimu. Wakapiga yowe,
Mark 6:49 in English
Mark 6:49 · Berean Standard Bible
but when they saw Him walking on the sea, they cried out, thinking He was a ghost—
Context
47Ilipofika jioni, ile mashua ilikuwa imefika katikati ya bahari, na Yesu alikuwa peke yake katika nchi kavu. 48Akawaona wanafunzi wake wanahangaika na kupiga makasia kwa nguvu, kwa sababu upepo ulikuwa wa mbisho. Wakati wa zamu ya nne ya usiku, Yesu akawaendea wanafunzi wake, akiwa anatembea juu ya maji. Alikuwa karibu kuwapita, 49lakini walipomwona akitembea juu ya maji, wakadhani ni mzimu. Wakapiga yowe, 50kwa sababu wote walipomwona waliogopa.
Mara Yesu akasema nao, akawaambia, “Jipeni moyo! Ni mimi. Msiogope!” 51Akapanda ndani ya mashua nao, na ule upepo ukakoma! Wakashangaa kabisa,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.