Marko 6:15
Mark 6:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wengine wakasema, “Yeye ni Eliya.” Nao wengine wakasema, “Yeye ni nabii, kama mmojawapo wa wale manabii wa zamani.”
Mark 6:15 in English
Mark 6:15 · Berean Standard Bible
Others were saying, “He is Elijah,” and still others, “He is a prophet, like one of the prophets of old.”
Context
13Wakatoa pepo wachafu wengi, wakawapaka wagonjwa wengi mafuta na kuwaponya. 14Mfalme Herode akasikia habari hizi, kwa maana jina la Yesu lilikuwa limejulikana sana. Watu wengine walikuwa wakisema, “Yohana Mbatizaji amefufuliwa kutoka kwa wafu, ndiyo sababu nguvu za kutenda miujiza zinafanya kazi ndani yake.” 15Wengine wakasema, “Yeye ni Eliya.”
Nao wengine wakasema, “Yeye ni nabii, kama mmojawapo wa wale manabii wa zamani.” 16Lakini Herode aliposikia habari hizi, akasema, “Huyo ni Yohana Mbatizaji, niliyemkata kichwa, amefufuliwa kutoka kwa wafu!” 17Kwa kuwa Herode alikuwa ameagiza kwamba Yohana Mbatizaji akamatwe, afungwe na kutiwa gerezani. Alifanya hivi kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo, ndugu yake, ambaye Herode alikuwa amemwoa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.