Marko 6:13
Mark 6:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wakatoa pepo wachafu wengi, wakawapaka wagonjwa wengi mafuta na kuwaponya.
Mark 6:13 in English
Mark 6:13 · Berean Standard Bible
They also drove out many demons and healed many of the sick, anointing them with oil.
Context
11Kama mahali popote hawatawakaribisha wala kuwasikiliza, mtakapoondoka huko, kungʼuteni mavumbi kutoka kwenye miguu yenu ili kuwa ushuhuda dhidi yao.” 12Kwa hiyo wakatoka na kuhubiri kwamba inawapasa watu kutubu na kuacha dhambi. 13Wakatoa pepo wachafu wengi, wakawapaka wagonjwa wengi mafuta na kuwaponya. 14Mfalme Herode akasikia habari hizi, kwa maana jina la Yesu lilikuwa limejulikana sana. Watu wengine walikuwa wakisema, “Yohana Mbatizaji amefufuliwa kutoka kwa wafu, ndiyo sababu nguvu za kutenda miujiza zinafanya kazi ndani yake.” 15Wengine wakasema, “Yeye ni Eliya.”
Nao wengine wakasema, “Yeye ni nabii, kama mmojawapo wa wale manabii wa zamani.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.