Marko 5:29
Mark 5:29 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mara kutoka damu kwake kukakoma, naye akajisikia mwilini mwake amepona kabisa.
Mark 5:29 in English
Mark 5:29 · Berean Standard Bible
Immediately her bleeding stopped, and she sensed in her body that she was healed of her affliction.
Context
27Alikuwa amesikia habari za Yesu, naye akaja kwa nyuma yake kwenye umati wa watu, akaligusa vazi lake, 28kwa maana alisema moyoni mwake, “Kama nikiweza kuligusa vazi lake tu, nitaponywa.” 29Mara kutoka damu kwake kukakoma, naye akajisikia mwilini mwake amepona kabisa. 30Ghafula Yesu akatambua kuwa nguvu zimemtoka. Akaugeukia ule umati wa watu na kuuliza, “Ni nani aliyegusa mavazi yangu?” 31Wanafunzi wake wakamjibu, “Unaona jinsi umati wa watu unavyokusonga. Wawezaje kuuliza, ‘Ni nani aliyenigusa?’ ”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.