Marko 5:2
Mark 5:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yesu alipotoka kwenye mashua, mara mtu mmoja mwenye pepo mchafu akatoka makaburini akakutana naye.
Mark 5:2 in English
Mark 5:2 · Berean Standard Bible
As soon as Jesus got out of the boat, He was met by a man with an unclean spirit, who was coming from the tombs.
Context
1Wakafika upande wa pili wa ziwa wakaingia katika nchi ya Wagerasi. 2Yesu alipotoka kwenye mashua, mara mtu mmoja mwenye pepo mchafu akatoka makaburini akakutana naye. 3Mtu huyu aliishi makaburini, wala hakuna aliyeweza kumzuia hata kwa kumfunga minyororo. 4Kwa kuwa mara kwa mara alikuwa amefungwa minyororo mikononi na miguuni, lakini akaikata hiyo minyororo na kuzivunja zile pingu miguuni mwake. Hapakuwa na mtu yeyote aliyekuwa na nguvu za kumzuia.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.