Marko 3:22
Mark 3:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Walimu wa sheria walioteremka kutoka Yerusalemu walisema, “Amepagawa na Beelzebuli!* Anatoa pepo wachafu kwa kutumia mkuu wa pepo wachafu!”
Mark 3:22 in English
Mark 3:22 · Berean Standard Bible
And the scribes who had come down from Jerusalem were saying, “He is possessed by Beelzebul,*” and, “By the prince of the demons He drives out demons.”
Context
20Kisha Yesu aliporudi nyumbani, umati wa watu ukakusanyika tena, kiasi kwamba yeye na wanafunzi wake hawakuweza kula chakula. 21Ndugu zake walipopata habari wakaja ili kumchukua kwa maana watu walikuwa wakisema, “Amerukwa na akili.” 22Walimu wa sheria walioteremka kutoka Yerusalemu walisema, “Amepagawa na Beelzebuli!* Anatoa pepo wachafu kwa kutumia mkuu wa pepo wachafu!” 23Basi Yesu akawaita na kuzungumza nao kwa mifano akasema: “Shetani awezaje kumtoa Shetani? 24Kama ufalme ukigawanyika dhidi yake wenyewe, ufalme huo hauwezi kusimama.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.