Native Bible

Mark 3:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ndugu zake walipopata habari wakaja ili kumchukua kwa maana watu walikuwa wakisema, “Amerukwa na akili.”

Mark 3:21 in English

Mark 3:21 · Berean Standard Bible

When His family heard about this, they went out to take custody of Him, saying, “He is out of His mind.”

Context

19na Yuda Iskariote aliyemsaliti Yesu. 20Kisha Yesu aliporudi nyumbani, umati wa watu ukakusanyika tena, kiasi kwamba yeye na wanafunzi wake hawakuweza kula chakula. 21Ndugu zake walipopata habari wakaja ili kumchukua kwa maana watu walikuwa wakisema, “Amerukwa na akili.” 22Walimu wa sheria walioteremka kutoka Yerusalemu walisema, “Amepagawa na Beelzebuli!* Anatoa pepo wachafu kwa kutumia mkuu wa pepo wachafu!” 23Basi Yesu akawaita na kuzungumza nao kwa mifano akasema: “Shetani awezaje kumtoa Shetani?

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.