Native Bible

Mark 15:36 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mtu mmoja akaenda mbio, akachovya sifongo kwenye siki, akaiweka kwenye mwanzi na akampa Yesu ili anywe, akisema, “Basi mwacheni. Hebu tuone kama Eliya atakuja kumshusha kutoka hapo msalabani.”

Mark 15:36 in English

Mark 15:36 · Berean Standard Bible

And someone ran and filled a sponge with sour wine.* He put it on a reed and held it up for Jesus to drink,* saying, “Leave Him alone. Let us see if Elijah comes to take Him down.”

Context

34Mnamo saa tisa, Yesu akapaza sauti, akalia, “Eloi, Eloi, lama sabakthani?” (maana yake, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”) 35Baadhi ya watu waliokuwa wamesimama karibu waliposikia hayo, wakasema, “Msikieni, anamwita Eliya.” 36Mtu mmoja akaenda mbio, akachovya sifongo kwenye siki, akaiweka kwenye mwanzi na akampa Yesu ili anywe, akisema, “Basi mwacheni. Hebu tuone kama Eliya atakuja kumshusha kutoka hapo msalabani.” 37Kisha Yesu akatoa sauti kuu, akakata roho. 38Pazia la Hekalu likachanika vipande viwili kuanzia juu hadi chini.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.