Marko 15:35
Mark 15:35 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Baadhi ya watu waliokuwa wamesimama karibu waliposikia hayo, wakasema, “Msikieni, anamwita Eliya.”
Mark 15:35 in English
Mark 15:35 · Berean Standard Bible
When some of those standing nearby heard this, they said, “Behold, He is calling Elijah.”
Context
33Ilipofika saa sita, giza liliifunika nchi yote hadi saa tisa. 34Mnamo saa tisa, Yesu akapaza sauti, akalia, “Eloi, Eloi, lama sabakthani?” (maana yake, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”) 35Baadhi ya watu waliokuwa wamesimama karibu waliposikia hayo, wakasema, “Msikieni, anamwita Eliya.” 36Mtu mmoja akaenda mbio, akachovya sifongo kwenye siki, akaiweka kwenye mwanzi na akampa Yesu ili anywe, akisema, “Basi mwacheni. Hebu tuone kama Eliya atakuja kumshusha kutoka hapo msalabani.” 37Kisha Yesu akatoa sauti kuu, akakata roho.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.