Native Bible

Mark 15:33 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ilipofika saa sita, giza liliifunika nchi yote hadi saa tisa.

Mark 15:33 in English

Mark 15:33 · Berean Standard Bible

From the sixth hour until the ninth hour * darkness came over all the land.

Context

31Vivyo hivyo, viongozi wa makuhani pamoja na walimu wa sheria wakamdhihaki miongoni mwao wakisema, “Aliwaokoa wengine, lakini hawezi kujiokoa mwenyewe! 32Basi huyu Kristo,* huyu Mfalme wa Israeli, ashuke sasa kutoka msalabani, ili tupate kuona na kuamini.” Wale waliosulubiwa pamoja naye pia wakamtukana. 33Ilipofika saa sita, giza liliifunika nchi yote hadi saa tisa. 34Mnamo saa tisa, Yesu akapaza sauti, akalia, “Eloi, Eloi, lama sabakthani?” (maana yake, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”) 35Baadhi ya watu waliokuwa wamesimama karibu waliposikia hayo, wakasema, “Msikieni, anamwita Eliya.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.