Marko 14:67
Mark 14:67 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Alipomwona Petro akiota moto, akamtazama sana, akamwambia, “Wewe pia ulikuwa pamoja na Yesu, Mnazareti.”
Mark 14:67 in English
Mark 14:67 · Berean Standard Bible
and saw him warming himself there. She looked at Peter and said, “You also were with Jesus the Nazarene.”
Context
65Kisha baadhi ya watu wakaanza kumtemea mate; wakamfunga kitambaa machoni, wakampiga kwa ngumi na kumwambia, “Tabiri!” Walinzi wakamchukua na kumpiga makofi. 66Petro alipokuwa bado yuko chini kwenye ua wa jumba la kifalme, tazama akaja mmoja wa watumishi wa kike wa kuhani mkuu. 67Alipomwona Petro akiota moto, akamtazama sana, akamwambia,
“Wewe pia ulikuwa pamoja na Yesu, Mnazareti.” 68Lakini Petro akakana, akasema, “Sijui wala sielewi unalosema.” Naye akaondoka kuelekea kwenye njia ya kuingilia. 69Yule mtumishi wa kike alipomwona mahali pale, akawaambia tena wale waliokuwa wamesimama hapo, “Huyu mtu ni mmoja wao.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.