Marko 14:5
Mark 14:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mafuta haya yangeweza kuuzwa kwa zaidi ya dinari* 300, na fedha hizo wakapewa maskini.” Wakamkemea vikali huyo mwanamke.
Mark 14:5 in English
Mark 14:5 · Berean Standard Bible
It could have been sold for over three hundred denarii * and the money given to the poor.” And they scolded her.
Context
3Yesu alikuwa Bethania nyumbani kwa Simoni aliyekuwa na ukoma. Wakati alipokuwa ameketi mezani akila chakula cha jioni, mwanamke mmoja aliingia akiwa na chupa ya marhamu yenye manukato ya nardo* safi ya thamani kubwa. Akaivunja hiyo chupa, akamiminia hayo manukato kichwani mwa Yesu. 4Baadhi ya watu waliokuwepo pale walikuwa wakisemezana wao kwa wao, “Upotevu huu wote ni wa nini? 5Mafuta haya yangeweza kuuzwa kwa zaidi ya dinari* 300, na fedha hizo wakapewa maskini.” Wakamkemea vikali huyo mwanamke. 6Lakini Yesu akawaambia, “Mbona mnamsumbua huyu mwanamke? Mwacheni! Yeye amenitendea jambo zuri sana. 7Maskini mtakuwa nao siku zote na mnaweza kuwasaidia wakati wowote mnaotaka. Lakini mimi hamtakuwa nami siku zote.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.