Marko 14:7
Mark 14:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Maskini mtakuwa nao siku zote na mnaweza kuwasaidia wakati wowote mnaotaka. Lakini mimi hamtakuwa nami siku zote.
Mark 14:7 in English
Mark 14:7 · Berean Standard Bible
The poor you will always have with you,* and you can help them whenever you want. But you will not always have Me.
Context
5Mafuta haya yangeweza kuuzwa kwa zaidi ya dinari* 300, na fedha hizo wakapewa maskini.” Wakamkemea vikali huyo mwanamke. 6Lakini Yesu akawaambia, “Mbona mnamsumbua huyu mwanamke? Mwacheni! Yeye amenitendea jambo zuri sana. 7Maskini mtakuwa nao siku zote na mnaweza kuwasaidia wakati wowote mnaotaka. Lakini mimi hamtakuwa nami siku zote. 8Huyu mwanamke amenitendea lile aliloweza. Ameumiminia mwili wangu manukato ili kuniandaa kwa maziko yangu. 9Amin, nawaambia, mahali popote ulimwenguni ambapo Injili itahubiriwa, jambo hili alilolitenda huyu mwanamke litatajwa pia kwa ukumbusho wake.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.