Marko 14:44
Mark 14:44 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Basi msaliti alikuwa amewapa hao watu ishara, kwamba: “Yule nitakayembusu ndiye. Mkamateni, mkamchukue chini ya ulinzi.”
Mark 14:44 in English
Mark 14:44 · Berean Standard Bible
Now the betrayer had arranged a signal with them: “The One I kiss is the man; arrest Him and lead Him away securely.”
Context
42Inukeni, twende zetu! Tazameni, msaliti wangu yuaja!” 43Yesu alipokuwa bado anazungumza, Yuda, mmoja wa wale wanafunzi Kumi na Wawili, akatokea. Alikuwa amefuatana na umati wa watu wenye panga na marungu, waliokuwa wametumwa na viongozi wa makuhani, walimu wa sheria, na wazee. 44Basi msaliti alikuwa amewapa hao watu ishara, kwamba: “Yule nitakayembusu ndiye. Mkamateni, mkamchukue chini ya ulinzi.” 45Mara Yuda akamjia Yesu na kusema, “Rabi.”* Akambusu. 46Wale watu wakamkamata Yesu, wakamweka chini ya ulinzi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.