Marko 13:29
Mark 13:29 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Vivyo hivyo, myaonapo mambo haya yakitukia, mnatambua kwamba wakati u karibu, hata malangoni.
Mark 13:29 in English
Mark 13:29 · Berean Standard Bible
So also, when you see these things happening, know that He is near,* right at the door.
Context
27Naye atawatuma malaika wake wawakusanye wateule wake kutoka pande zote nne za dunia, kutoka miisho ya dunia hadi miisho ya mbingu. 28“Basi jifunzeni somo hili kutokana na mtini: Matawi yake yanapoanza kuchipua na kutoa majani, mnatambua kwamba wakati wa kiangazi umekaribia. 29Vivyo hivyo, myaonapo mambo haya yakitukia, mnatambua kwamba wakati u karibu, hata malangoni. 30Amin, nawaambia, kizazi hiki hakitapita hadi mambo haya yote yawe yametimia. 31Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.