Marko 11:8
Mark 11:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Watu wengi wakatandaza mavazi yao barabarani, na wengine wakatandaza matawi waliyokuwa wamekata mashambani.
Mark 11:8 in English
Mark 11:8 · Berean Standard Bible
Many in the crowd spread their cloaks on the road, while others spread branches they had cut from the fields.
Context
6Wakawajibu kama vile Yesu alivyokuwa amewaagiza, nao wale watu wakawaruhusu. 7Kisha wakamleta huyo mwana-punda kwa Yesu na kutandika mavazi yao juu yake, naye akampanda. 8Watu wengi wakatandaza mavazi yao barabarani, na wengine wakatandaza matawi waliyokuwa wamekata mashambani. 9Kisha wale waliokuwa wametangulia mbele na wale waliokuwa wakifuata nyuma wakapaza sauti, wakisema,
“Hosana!”*
“Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Bwana!” 10“Umebarikiwa Ufalme unaokuja wa baba yetu Daudi!”
“Hosana kwake yeye aliye juu!”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.