Native Bible

Mark 10:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Watu walikuwa wakimletea Yesu watoto wadogo ili awaguse, lakini wanafunzi wake wakawakemea.

Mark 10:13 in English

Mark 10:13 · Berean Standard Bible

Now people were bringing the little children to Jesus for Him to place His hands on them, and the disciples rebuked those who brought them.

Context

11Akawajibu, “Mtu yeyote amwachaye mkewe na kuoa mke mwingine, anazini naye. 12Naye mwanamke amwachaye mumewe na kuolewa na mume mwingine, anazini.” 13Watu walikuwa wakimletea Yesu watoto wadogo ili awaguse, lakini wanafunzi wake wakawakemea. 14Yesu alipoona yaliyokuwa yakitukia, akachukizwa. Akawaambia wanafunzi wake, “Waacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana Ufalme wa Mungu ni wa wale walio kama hawa. 15Amin, nawaambia, mtu yeyote asiyeupokea Ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo, hatauingia kamwe.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.