Marko 1:25
Mark 1:25 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini Yesu akamkemea, akamwambia, “Nyamaza kimya! Nawe umtoke!”
Mark 1:25 in English
Mark 1:25 · Berean Standard Bible
But Jesus rebuked the spirit. “Be silent!” He said. “Come out of him!”
Context
23Wakati huo huo katika sinagogi lao palikuwa na mtu aliyekuwa amepagawa na pepo mchafu, 24naye akapiga kelele akisema, “Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti? Je, umekuja kutuangamiza? Ninakujua wewe ni nani. Wewe ndiwe Aliye Mtakatifu wa Mungu!” 25Lakini Yesu akamkemea, akamwambia, “Nyamaza kimya! Nawe umtoke!” 26Yule pepo mchafu akamtikisatikisa huyo mtu kwa nguvu, kisha akamtoka akipiga kelele kwa sauti kubwa. 27Watu wote wakashangaa, hata wakaulizana wao kwa wao, “Haya ni mambo gani? Ni mafundisho mapya, tena yenye mamlaka! Anaamuru hata pepo wachafu, nao wanamtii!”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.