Native Bible

Mark 1:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Yule pepo mchafu akamtikisatikisa huyo mtu kwa nguvu, kisha akamtoka akipiga kelele kwa sauti kubwa.

Mark 1:26 in English

Mark 1:26 · Berean Standard Bible

At this, the unclean spirit threw the man into convulsions and came out with a loud shriek.

Context

24naye akapiga kelele akisema, “Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti? Je, umekuja kutuangamiza? Ninakujua wewe ni nani. Wewe ndiwe Aliye Mtakatifu wa Mungu!” 25Lakini Yesu akamkemea, akamwambia, “Nyamaza kimya! Nawe umtoke!” 26Yule pepo mchafu akamtikisatikisa huyo mtu kwa nguvu, kisha akamtoka akipiga kelele kwa sauti kubwa. 27Watu wote wakashangaa, hata wakaulizana wao kwa wao, “Haya ni mambo gani? Ni mafundisho mapya, tena yenye mamlaka! Anaamuru hata pepo wachafu, nao wanamtii!” 28Sifa zake zikaanza kuenea haraka katika eneo lote la karibu na Galilaya.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.