Native Bible

Micah 4:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwa nini sasa unalia kwa nguvu: kwani huna mfalme? Je, mshauri wako amekufa, hata maumivu yakukamate kama ya mwanamke aliye na utungu wa kuzaa?

Micah 4:9 in English

Micah 4:9 · Berean Standard Bible

Why do you now cry aloud? Is there no king among you? Has your counselor perished so that anguish grips you like a woman in labor?

Context

7Nitawafanya walemavu kuwa mabaki, wale waliofukuzwa kuwa taifa lenye nguvu. Bwana atatawala juu yao katika Mlima Sayuni kuanzia siku hiyo na hata milele. 8Lakini kuhusu wewe, ee mnara wa ulinzi wa kundi, ee ngome ya Binti Sayuni, milki ya awali itarudishwa kwako, ufalme utakuja kwa Binti Yerusalemu.” 9Kwa nini sasa unalia kwa nguvu: kwani huna mfalme? Je, mshauri wako amekufa, hata maumivu yakukamate kama ya mwanamke aliye na utungu wa kuzaa? 10Gaagaa kwa utungu, ee Binti Sayuni, kama mwanamke mwenye utungu wa kuzaa, kwa kuwa sasa ni lazima uuache mji ukapige kambi uwanjani. Utakwenda Babeli; huko utaokolewa. Huko Bwana atakukomboa kutoka mikononi mwa adui zako. 11Lakini sasa mataifa mengi yamekusanyika dhidi yako. Wanasema, “Mwache anajisiwe, macho yetu na yatazame Sayuni kwa furaha!”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.