Native Bible

Micah 4:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mataifa yote yanaweza kutembea katika jina la miungu yao; sisi tutatembea katika jina la Bwana Mungu wetu milele na milele.

Micah 4:5 in English

Micah 4:5 · Berean Standard Bible

Though each of the peoples may walk in the name of his god, yet we will walk in the name of the LORD our God forever and ever.

Context

3Atahukumu kati ya mataifa mengi, na ataamua migogoro ya mataifa yenye nguvu na yaliyo mbali. Watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao kuwa miundu ya kukata matawi. Taifa halitainua upanga dhidi ya taifa jingine, wala hawatajifunza vita tena. 4Kila mtu ataketi chini ya mzabibu wake na chini ya mtini wake, wala hakuna mtu atakayewaogopesha, kwa kuwa Bwana Mwenye Nguvu Zote amesema. 5Mataifa yote yanaweza kutembea katika jina la miungu yao; sisi tutatembea katika jina la Bwana Mungu wetu milele na milele. 6“Katika siku hiyo,” asema Bwana, “nitawakusanya walemavu; nitawakusanya walio uhamishoni na wale niliowahuzunisha. 7Nitawafanya walemavu kuwa mabaki, wale waliofukuzwa kuwa taifa lenye nguvu. Bwana atatawala juu yao katika Mlima Sayuni kuanzia siku hiyo na hata milele.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.