Native Bible

Matthew 9:29 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ndipo Yesu akagusa macho yao na kusema, “Iwe kwenu sawasawa na imani yenu.”

Matthew 9:29 in English

Matthew 9:29 · Berean Standard Bible

Then He touched their eyes and said, “According to your faith will it be done to you.”

Context

27Yesu alipokuwa akiondoka mahali pale, vipofu wawili wakamfuata wakipiga kelele kwa nguvu na kusema, “Mwana wa Daudi, tuhurumie!” 28Alipoingia mle nyumbani wale vipofu wakamjia. Naye Yesu akawauliza, “Mnaamini kwamba ninaweza kufanya jambo hili?” Wakamjibu, “Ndiyo, Bwana.” 29Ndipo Yesu akagusa macho yao na kusema, “Iwe kwenu sawasawa na imani yenu.” 30Macho yao yakafunguka. Yesu akawaonya vikali, akisema, “Angalieni mtu yeyote asijue kuhusu jambo hili.” 31Lakini wao wakaenda na kueneza habari zake katika eneo lile lote.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.