Mathayo 5:43
Matthew 5:43 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Mmesikia kwamba ilinenwa, ‘Mpende jirani yako na umchukie adui yako.’
Matthew 5:43 in English
Matthew 5:43 · Berean Standard Bible
You have heard that it was said, ‘Love your neighbor’* and ‘Hate your enemy.’
Context
41Kama mtu akikulazimisha kwenda maili moja, nenda naye maili mbili. 42Mpe yeye akuombaye, wala usimgeuzie kisogo yeye atakaye kukukopa. 43“Mmesikia kwamba ilinenwa, ‘Mpende jirani yako na umchukie adui yako.’ 44Lakini ninawaambia: Wapendeni adui zenu na waombeeni wanaowatesa ninyi, 45ili mpate kuwa watoto wa Baba yenu aliye mbinguni. Kwa maana yeye huwaangazia jua lake watu waovu na watu wema, naye huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.