Mathayo 4:3
Matthew 4:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mjaribu akamjia na kumwambia, “Ikiwa wewe ndiye Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate.”
Matthew 4:3 in English
Matthew 4:3 · Berean Standard Bible
The tempter came to Him and said, “If You are the Son of God, tell these stones to become bread.”
Context
1Kisha Yesu akaongozwa na Roho Mtakatifu kwenda nyikani ili akajaribiwe na ibilisi. 2Baada ya kufunga siku arobaini usiku na mchana, hatimaye akaona njaa. 3Mjaribu akamjia na kumwambia, “Ikiwa wewe ndiye Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate.” 4Lakini Yesu akajibu, “Imeandikwa: ‘Mtu haishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.’ ” 5Ndipo ibilisi akamchukua Yesu mpaka mji mtakatifu na kumweka juu ya mnara mrefu wa Hekalu,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.