Mathayo 27:23
Matthew 27:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Pilato akauliza, “Kwa nini? Amefanya kosa gani?” Lakini wao wakazidi kupiga kelele, wakisema, “Msulubishe!”
Matthew 27:23 in English
Matthew 27:23 · Berean Standard Bible
“Why?” asked Pilate. “What evil has He done?” But they shouted all the louder, “Crucify Him!”
Context
21Mtawala akawauliza tena, “Ni yupi kati ya hawa wawili mnayetaka niwafungulie?”
Wakajibu, “Baraba.” 22Pilato akawaambia, “Basi nifanye nini na huyu Yesu aitwaye Kristo?”
Wakajibu wote, “Msulubishe!” 23Pilato akauliza, “Kwa nini? Amefanya kosa gani?”
Lakini wao wakazidi kupiga kelele, wakisema, “Msulubishe!” 24Pilato alipoona kwamba hawezi kufanya lolote, lakini badala yake ghasia zilikuwa zinaanza, akachukua maji, akanawa mikono yake mbele ya ule umati wa watu, akasema, “Sina hatia juu ya damu ya mtu huyu, hili ni jukumu lenu!” 25Watu wote wakajibu, “Damu yake na iwe juu yetu na juu ya watoto wetu!”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.