Mathayo 25:14
Matthew 25:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Tena, Ufalme wa Mbinguni ni kama mtu aliyetaka kusafiri, naye akawaita watumishi wake na kuweka mali yake kwenye uangalizi wao.
Matthew 25:14 in English
Matthew 25:14 · Berean Standard Bible
For it is just like a man going on a journey, who called his servants and entrusted them with his possessions.
Context
12“Lakini yeye bwana arusi akawajibu, ‘Amin, amin nawaambia, siwajui ninyi!’ 13“Kwa hiyo kesheni, kwa sababu hamjui siku wala saa. 14“Tena, Ufalme wa Mbinguni ni kama mtu aliyetaka kusafiri, naye akawaita watumishi wake na kuweka mali yake kwenye uangalizi wao. 15Mmoja akampa talanta* tano, mwingine talanta mbili, na mwingine talanta moja. Kila mmoja alipewa kwa kadiri ya uwezo wake. Kisha yeye akasafiri. 16Yule aliyepewa talanta tano akaenda mara moja akafanya nazo biashara akapata talanta nyingine tano zaidi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.