Native Bible

Matthew 22:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwa hiyo nendeni katika njia panda mkamwalike karamuni yeyote mtakayemwona.’

Matthew 22:9 in English

Matthew 22:9 · Berean Standard Bible

Go therefore to the crossroads and invite to the banquet as many as you can find.’

Context

7Yule mfalme akakasirika sana, akapeleka jeshi lake likawaangamiza wale wauaji na kuuteketeza mji wao kwa moto. 8“Kisha akawaambia watumishi wake, ‘Karamu ya arusi imeshakuwa tayari, lakini wale niliowaalika hawakustahili kuja. 9Kwa hiyo nendeni katika njia panda mkamwalike karamuni yeyote mtakayemwona.’ 10Wale watumishi wakaenda barabarani, wakawakusanya watu wote waliowaona, wema na wabaya. Ukumbi wa arusi ukajaa wageni. 11“Lakini mfalme alipoingia ndani ili kuwaona wageni, akamwona mle mtu mmoja ambaye hakuwa amevaa vazi la arusi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.