Mathayo 22:11
Matthew 22:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Lakini mfalme alipoingia ndani ili kuwaona wageni, akamwona mle mtu mmoja ambaye hakuwa amevaa vazi la arusi.
Matthew 22:11 in English
Matthew 22:11 · Berean Standard Bible
But when the king came in to see the guests, he spotted a man who was not dressed in wedding clothes.
Context
9Kwa hiyo nendeni katika njia panda mkamwalike karamuni yeyote mtakayemwona.’ 10Wale watumishi wakaenda barabarani, wakawakusanya watu wote waliowaona, wema na wabaya. Ukumbi wa arusi ukajaa wageni. 11“Lakini mfalme alipoingia ndani ili kuwaona wageni, akamwona mle mtu mmoja ambaye hakuwa amevaa vazi la arusi. 12Mfalme akamuuliza, ‘Rafiki, uliingiaje humu bila vazi la arusi?’ Yule mtu hakuwa na la kusema. 13“Ndipo mfalme akawaambia watumishi wake, ‘Mfungeni mikono na miguu mkamtupe nje, kwenye giza. Huko kutakuwa na kilio na kusaga meno.’
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.