Mathayo 21:43
Matthew 21:43 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Kwa hiyo ninawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu na kupewa watu wengine wawezao kuzaa matunda yake.
Matthew 21:43 in English
Matthew 21:43 · Berean Standard Bible
Therefore I tell you that the kingdom of God will be taken away from you and given to a people who will produce its fruit.
Context
41Wakamjibu, “Kwa huzuni kuu atawaangamiza kabisa hao wadhalimu na kulipangisha shamba lake la mizabibu kwa wakulima wengine ambao watampatia fungu lake la matunda wakati wa mavuno.” 42Yesu akawaambia, “Je, hamjasoma katika Maandiko kwamba:
“ ‘Jiwe walilolikataa waashi
limekuwa jiwe kuu la pembeni.
Bwana ndiye alitenda jambo hili,
nalo ni la ajabu machoni petu’? 43“Kwa hiyo ninawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu na kupewa watu wengine wawezao kuzaa matunda yake. 44Yeye aangukaye juu ya jiwe hili atavunjika vipande vipande, lakini yule litakayemwangukia atasagwa kabisa.” 45Viongozi wa Makuhani na Mafarisayo waliposikia mifano ya Yesu, walitambua kuwa alikuwa akiwasema wao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.