Native Bible

Matthew 2:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ndipo lilipotimia neno lililonenwa na nabii Yeremia.

Matthew 2:17 in English

Matthew 2:17 · Berean Standard Bible

Then what was spoken through the prophet Jeremiah was fulfilled:

Context

15ambako walikaa mpaka Herode alipofariki. Hili lilifanyika ili litimie lile lililonenwa na Bwana kwa kinywa cha nabii kusema: “Nilimwita mwanangu kutoka Misri.” 16Herode alipongʼamua kwamba wale wataalamu wa nyota wamemshinda kwa akili, alikasirika sana, naye akatoa amri ya kuwaua watoto wote wa kiume wenye umri wa miaka miwili kurudi chini katika mji wa Bethlehemu na sehemu zote za jirani, kufuatana na ule muda alioambiwa na wale wataalamu wa nyota. 17Ndipo lilipotimia neno lililonenwa na nabii Yeremia. 18“Sauti ilisikika huko Rama, maombolezo na kilio kikubwa, Raheli akilia kwa ajili ya wanawe, akikataa kufarijiwa, kwa sababu hawako tena.” 19Baada ya Herode kufa, malaika wa Bwana akamtokea Yosefu katika ndoto huko Misri

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.