Mathayo 19:15
Matthew 19:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Naye akaweka mikono yake juu yao, na akaondoka huko.
Matthew 19:15 in English
Matthew 19:15 · Berean Standard Bible
And after He had placed His hands on them, He went on from there.
Context
13Kisha watoto wadogo wakaletwa kwa Yesu ili aweke mikono yake juu yao na awaombee. Lakini wanafunzi wake wakawakemea wale waliowaleta. 14Yesu akasema, “Waacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana Ufalme wa Mbinguni ni wa wale walio kama hawa.” 15Naye akaweka mikono yake juu yao, na akaondoka huko. 16Mtu mmoja akamjia Yesu na kumuuliza, “Mwalimu mwema, nifanye jambo gani jema ili nipate uzima wa milele?” 17Yesu akamjibu, “Mbona unaniuliza habari ya mema? Aliye mwema ni Mmoja tu. Lakini ukitaka kuingia uzimani, zitii amri.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.