Mathayo 18:22
Matthew 18:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yesu akamjibu, “Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini.
Matthew 18:22 in English
Matthew 18:22 · Berean Standard Bible
Jesus answered, “I tell you, not just seven times, but seventy-seven times!*
Context
20Kwa kuwa wanapokusanyika pamoja watu wawili au watatu kwa Jina langu, mimi niko papo hapo pamoja nao.” 21Ndipo Petro akamjia Yesu na kumuuliza, “Bwana, ndugu yangu anikosee mara ngapi nami nimsamehe? Je, hata mara saba?” 22Yesu akamjibu, “Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini. 23“Kwa hiyo Ufalme wa Mbinguni unaweza kufananishwa na mfalme aliyetaka kufanya hesabu zake za fedha na watumishi wake. 24Alipoanza kufanya hesabu zake, mtu mmoja aliyekuwa anadaiwa talanta* 10,000, aliletwa kwake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.