Mathayo 17:24
Matthew 17:24 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Baada ya Yesu na wanafunzi wake kufika Kapernaumu, wakusanya kodi ya Hekalu* wakamjia Petro na kumuuliza, “Je, Mwalimu wenu halipi kodi ya Hekalu?”
Matthew 17:24 in English
Matthew 17:24 · Berean Standard Bible
After they had arrived in Capernaum, the collectors of the two-drachma tax * came to Peter and asked, “Does your Teacher pay the two drachmas?”
Context
22Siku moja walipokuwa pamoja huko Galilaya, Yesu akawaambia, “Mwana wa Adamu atasalitiwa na kutiwa mikononi mwa watu. 23Nao watamuua, lakini siku ya tatu atafufuliwa.” Wanafunzi wakahuzunika sana. 24Baada ya Yesu na wanafunzi wake kufika Kapernaumu, wakusanya kodi ya Hekalu* wakamjia Petro na kumuuliza, “Je, Mwalimu wenu halipi kodi ya Hekalu?” 25Petro akajibu, “Ndiyo, yeye hulipa.” Petro aliporudi nyumbani, Yesu akawa wa kwanza kulizungumzia, akamuuliza, “Unaonaje Simoni? Wafalme wa dunia hupokea ushuru na kodi kutoka kwa nani? Je, ni kutoka kwa watoto wao au kutoka kwa watu wengine?” 26Petro akamjibu, “Kutoka kwa watu wengine.” Yesu akamwambia, “Kwa hiyo watoto wao wamesamehewa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.