Native Bible

Matthew 17:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Nao watamuua, lakini siku ya tatu atafufuliwa.” Wanafunzi wakahuzunika sana.

Matthew 17:23 in English

Matthew 17:23 · Berean Standard Bible

They will kill Him, and on the third day He will be raised to life.” And the disciples were deeply grieved.

Context

21Lakini hali kama hii haitoki ila kwa kuomba na kufunga.]” 22Siku moja walipokuwa pamoja huko Galilaya, Yesu akawaambia, “Mwana wa Adamu atasalitiwa na kutiwa mikononi mwa watu. 23Nao watamuua, lakini siku ya tatu atafufuliwa.” Wanafunzi wakahuzunika sana. 24Baada ya Yesu na wanafunzi wake kufika Kapernaumu, wakusanya kodi ya Hekalu* wakamjia Petro na kumuuliza, “Je, Mwalimu wenu halipi kodi ya Hekalu?” 25Petro akajibu, “Ndiyo, yeye hulipa.” Petro aliporudi nyumbani, Yesu akawa wa kwanza kulizungumzia, akamuuliza, “Unaonaje Simoni? Wafalme wa dunia hupokea ushuru na kodi kutoka kwa nani? Je, ni kutoka kwa watoto wao au kutoka kwa watu wengine?”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.