Mathayo 14:31
Matthew 14:31 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mara Yesu akaunyoosha mkono wake na kumshika, akamwambia, “Wewe mwenye imani haba, kwa nini uliona shaka?”
Matthew 14:31 in English
Matthew 14:31 · Berean Standard Bible
Immediately Jesus reached out His hand and took hold of Peter. “You of little faith,” He said, “why did you doubt?”
Context
29Yesu akamwambia, “Njoo.”
Basi Petro akatoka kwenye chombo, akatembea juu ya maji kumwelekea Yesu. 30Lakini alipoona upepo mkali aliingiwa na hofu, naye akaanza kuzama, huku akipiga kelele, “Bwana, niokoe!” 31Mara Yesu akaunyoosha mkono wake na kumshika, akamwambia, “Wewe mwenye imani haba, kwa nini uliona shaka?” 32Nao walipoingia ndani ya mashua, upepo ukakoma. 33Ndipo wote waliokuwa ndani ya ile mashua wakamwabudu Yesu, wakisema, “Hakika, wewe ndiwe Mwana wa Mungu.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.