Native Bible

Matthew 14:30 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Lakini alipoona upepo mkali aliingiwa na hofu, naye akaanza kuzama, huku akipiga kelele, “Bwana, niokoe!”

Matthew 14:30 in English

Matthew 14:30 · Berean Standard Bible

But when he saw the strength of the wind,* he was afraid, and beginning to sink, cried out, “Lord, save me!”

Context

28Petro akamjibu, “Bwana, ikiwa ni wewe, niambie nije kwako nikitembea juu ya maji.” 29Yesu akamwambia, “Njoo.” Basi Petro akatoka kwenye chombo, akatembea juu ya maji kumwelekea Yesu. 30Lakini alipoona upepo mkali aliingiwa na hofu, naye akaanza kuzama, huku akipiga kelele, “Bwana, niokoe!” 31Mara Yesu akaunyoosha mkono wake na kumshika, akamwambia, “Wewe mwenye imani haba, kwa nini uliona shaka?” 32Nao walipoingia ndani ya mashua, upepo ukakoma.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.