Mathayo 14:27
Matthew 14:27 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini mara Yesu akasema nao, akawaambia, “Jipeni moyo! Ni mimi. Msiogope.”
Matthew 14:27 in English
Matthew 14:27 · Berean Standard Bible
But Jesus spoke up at once: “Take courage! It is I. Do not be afraid.”
Context
25Wakati wa zamu ya nne ya usiku,* Yesu akawaendea wanafunzi wake akiwa anatembea juu ya maji. 26Wanafunzi wake walipomwona akitembea juu ya maji, waliingiwa na hofu kuu, wakasema, “Ni mzimu.” Wakapiga yowe kwa kuogopa. 27Lakini mara Yesu akasema nao, akawaambia, “Jipeni moyo! Ni mimi. Msiogope.” 28Petro akamjibu, “Bwana, ikiwa ni wewe, niambie nije kwako nikitembea juu ya maji.” 29Yesu akamwambia, “Njoo.”
Basi Petro akatoka kwenye chombo, akatembea juu ya maji kumwelekea Yesu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.