Native Bible

Matthew 14:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wanafunzi wake walipomwona akitembea juu ya maji, waliingiwa na hofu kuu, wakasema, “Ni mzimu.” Wakapiga yowe kwa kuogopa.

Matthew 14:26 in English

Matthew 14:26 · Berean Standard Bible

When the disciples saw Him walking on the sea, they were terrified. “It’s a ghost!” they said, and cried out in fear.

Context

24Wakati huo ile mashua ilikuwa mbali kutoka nchi kavu ikisukwasukwa na mawimbi, kwa sababu upepo ulikuwa wa mbisho. 25Wakati wa zamu ya nne ya usiku,* Yesu akawaendea wanafunzi wake akiwa anatembea juu ya maji. 26Wanafunzi wake walipomwona akitembea juu ya maji, waliingiwa na hofu kuu, wakasema, “Ni mzimu.” Wakapiga yowe kwa kuogopa. 27Lakini mara Yesu akasema nao, akawaambia, “Jipeni moyo! Ni mimi. Msiogope.” 28Petro akamjibu, “Bwana, ikiwa ni wewe, niambie nije kwako nikitembea juu ya maji.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.