Native Bible

Matthew 14:25 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wakati wa zamu ya nne ya usiku,* Yesu akawaendea wanafunzi wake akiwa anatembea juu ya maji.

Matthew 14:25 in English

Matthew 14:25 · Berean Standard Bible

During the fourth watch of the night,* Jesus went out to them, walking on the sea.

Context

23Baada ya kuwaaga, akaenda zake mlimani peke yake kuomba. Jioni ilipofika, Yesu alikuwa huko peke yake. 24Wakati huo ile mashua ilikuwa mbali kutoka nchi kavu ikisukwasukwa na mawimbi, kwa sababu upepo ulikuwa wa mbisho. 25Wakati wa zamu ya nne ya usiku,* Yesu akawaendea wanafunzi wake akiwa anatembea juu ya maji. 26Wanafunzi wake walipomwona akitembea juu ya maji, waliingiwa na hofu kuu, wakasema, “Ni mzimu.” Wakapiga yowe kwa kuogopa. 27Lakini mara Yesu akasema nao, akawaambia, “Jipeni moyo! Ni mimi. Msiogope.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.