Mathayo 14:17
Matthew 14:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wakamjibu, “Tuna mikate mitano na samaki wawili tu.”
Matthew 14:17 in English
Matthew 14:17 · Berean Standard Bible
“We have here only five loaves of bread and two fish,” they answered.
Context
15Ilipofika jioni, wanafunzi wake walienda kwake, wakamwambia, “Mahali hapa ni nyikani, na muda sasa umekwisha. Waage makutano ili waende zao vijijini wakajinunulie chakula.” 16Yesu akawaambia, “Hakuna sababu ya wao kuondoka. Ninyi wapeni chakula.” 17Wakamjibu, “Tuna mikate mitano na samaki wawili tu.” 18Akawaambia, “Nileteeni hivyo vitu hapa.” 19Yesu akaagiza makutano wakae chini kwenye nyasi. Akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili, akainua macho yake akatazama mbinguni, akavibariki na kuimega ile mikate. Kisha akawapa wanafunzi, nao wanafunzi wakawagawia makutano.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.