Mathayo 13:52
Matthew 13:52 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Akawaambia, “Basi kila mwalimu wa sheria aliyefundishwa elimu ya Ufalme wa Mbinguni ni kama mwenye nyumba anayetoa kutoka ghala yake mali mpya na mali ya zamani.”
Matthew 13:52 in English
Matthew 13:52 · Berean Standard Bible
Then He told them, “For this reason, every scribe who has been discipled in the kingdom of heaven is like a homeowner who brings out of his storeroom new treasures as well as old.”
Context
50Nao watawatupa hao waovu katika tanuru la moto ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno.” 51Yesu akauliza, “Je, mmeyaelewa haya yote?”
Wakamjibu, “Ndiyo.” 52Akawaambia, “Basi kila mwalimu wa sheria aliyefundishwa elimu ya Ufalme wa Mbinguni ni kama mwenye nyumba anayetoa kutoka ghala yake mali mpya na mali ya zamani.” 53Yesu alipomaliza kutoa mifano hii, akaondoka. 54Alipofika mji wa kwao, akawafundisha watu katika sinagogi lao. Nao wakastaajabu, wakauliza, “Mtu huyu amepata wapi hekima hii na uwezo huu wa kufanya miujiza?”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.