Mathayo 13:49
Matthew 13:49 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hivi ndivyo itakavyokuwa wakati wa mwisho wa dunia. Malaika watakuja na kuwatenganisha watu waovu na watu wenye haki.
Matthew 13:49 in English
Matthew 13:49 · Berean Standard Bible
So will it be at the end of the age: The angels will come and separate the wicked from the righteous,
Context
47“Tena, Ufalme wa Mbinguni ni kama wavu wa kuvua samaki uliotupwa baharini ukavua samaki wa kila aina. 48Ulipojaa, wavuvi wakavuta pwani, wakaketi na kukusanya samaki wazuri kuwaweka kwenye vyombo safi, lakini wale samaki wabaya wakawatupa. 49Hivi ndivyo itakavyokuwa wakati wa mwisho wa dunia. Malaika watakuja na kuwatenganisha watu waovu na watu wenye haki. 50Nao watawatupa hao waovu katika tanuru la moto ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno.” 51Yesu akauliza, “Je, mmeyaelewa haya yote?”
Wakamjibu, “Ndiyo.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.