Native Bible

Matthew 13:41 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutoka Ufalme wake kila kitu kinachosababisha dhambi na watenda maovu wote.

Matthew 13:41 in English

Matthew 13:41 · Berean Standard Bible

The Son of Man will send out His angels, and they will weed out of His kingdom every cause of sin and all who practice lawlessness.

Context

39Yule adui aliyepanda magugu ni ibilisi. Mavuno ni mwisho wa dunia, nao wavunaji ni malaika. 40“Kama vile magugu yangʼolewavyo na kuchomwa motoni, ndivyo itakavyokuwa wakati wa mwisho wa dunia. 41Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutoka Ufalme wake kila kitu kinachosababisha dhambi na watenda maovu wote. 42Nao watawatupa katika tanuru la moto ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno. 43Ndipo wenye haki watangʼaa kama jua katika Ufalme wa Baba yao. Yeye aliye na masikio, na asikie.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.