Native Bible

Matthew 13:42 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Nao watawatupa katika tanuru la moto ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno.

Matthew 13:42 in English

Matthew 13:42 · Berean Standard Bible

And they will throw them into the fiery furnace, where there will be weeping and gnashing of teeth.

Context

40“Kama vile magugu yangʼolewavyo na kuchomwa motoni, ndivyo itakavyokuwa wakati wa mwisho wa dunia. 41Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutoka Ufalme wake kila kitu kinachosababisha dhambi na watenda maovu wote. 42Nao watawatupa katika tanuru la moto ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno. 43Ndipo wenye haki watangʼaa kama jua katika Ufalme wa Baba yao. Yeye aliye na masikio, na asikie. 44“Ufalme wa Mbinguni unafanana na hazina iliyofichwa shambani, ambayo mtu mmoja alipoiona akaificha tena. Kisha katika furaha yake, akaenda akauza vyote alivyokuwa navyo, akalinunua lile shamba.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.