Mathayo 13:2
Matthew 13:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Umati mkubwa mno wa watu ukakusanyika kumzunguka, hata ikabidi aingie katika chombo na kuketi humo, nao watu wote wakawa wamesimama ukingoni mwa bahari.
Matthew 13:2 in English
Matthew 13:2 · Berean Standard Bible
Such large crowds gathered around Him that He got into a boat and sat down, while all the people stood on the shore.
Context
1Siku iyo hiyo Yesu akatoka nje ya nyumba, akaketi kando ya bahari. 2Umati mkubwa mno wa watu ukakusanyika kumzunguka, hata ikabidi aingie katika chombo na kuketi humo, nao watu wote wakawa wamesimama ukingoni mwa bahari. 3Ndipo akawaambia mambo mengi kwa mifano, akisema: “Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu zake. 4Alipokuwa akitawanya mbegu, nyingine zilianguka kando ya njia, nao ndege wakaja na kuzila.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.