Malaki 1:7
Malachi 1:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Mnatoa sadaka chakula kilichotiwa unajisi juu ya madhabahu yangu. “Lakini ninyi mnauliza, ‘Tumekutia unajisi kwa namna gani?’ “Kwa kusema kuwa meza ya Bwana ni ya kudharauliwa.
Malachi 1:7 in English
Malachi 1:7 · Berean Standard Bible
By presenting defiled food on My altar. But you ask, ‘How have we defiled You *?’ By saying that the table of the LORD is contemptible.
Context
5Mtayaona kwa macho yenu wenyewe na kusema, ‘Bwana ni mkuu, hata nje ya mipaka ya Israeli!’ 6“Mwana humheshimu baba yake, naye mtumishi humheshimu bwana wake. Kama mimi ni baba, iko wapi heshima ninayostahili? Kama mimi ni bwana, iko wapi heshima ninayostahili?” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote. “Ni ninyi, enyi makuhani, mnaolidharau Jina langu.
“Lakini mnauliza, ‘Tumelidharau Jina lako kwa namna gani?’ 7“Mnatoa sadaka chakula kilichotiwa unajisi juu ya madhabahu yangu.
“Lakini ninyi mnauliza, ‘Tumekutia unajisi kwa namna gani?’
“Kwa kusema kuwa meza ya Bwana ni ya kudharauliwa. 8Wakati mletapo dhabihu za wanyama walio vipofu, je, hilo si kosa? Mnapoleta dhabihu zilizo vilema au wanyama wagonjwa, je, hilo si kosa? Jaribuni kuvitoa kwa mtawala wenu! Je, angefurahishwa nanyi? Je, atawakubalia?” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote. 9“Basi mwombeni Mungu awe na neema kwetu. Je, kwa sadaka kama hizo kutoka mikononi mwenu, atawapokea?” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.