Luka 9:3
Luke 9:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Akawaagiza akisema, “Msichukue chochote safarini: sio fimbo, wala mkoba, wala mkate, wala fedha, hata msichukue kanzu ya ziada.
Luke 9:3 in English
Luke 9:3 · Berean Standard Bible
“Take nothing for the journey,” He told them, “no staff, no bag, no bread, no money,* no second tunic.
Context
1Yesu kisha akawaita wale kumi na wawili pamoja, akawapa mamlaka na uwezo wa kutoa pepo wachafu wote na kuponya magonjwa yote, 2kisha akawatuma waende wakahubiri Ufalme wa Mungu na kuponya wagonjwa. 3Akawaagiza akisema, “Msichukue chochote safarini: sio fimbo, wala mkoba, wala mkate, wala fedha, hata msichukue kanzu ya ziada. 4Katika nyumba yoyote mwingiayo, kaeni humo hadi mtakapoondoka katika mji huo. 5Kama watu wasipowakaribisha, mnapoondoka katika mji wao, kungʼuteni mavumbi kutoka kwenye miguu yenu ili kuwa ushuhuda dhidi yao.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.